IPO HAJA KWA WAZAZI NA WALEZI KUA NA USHIRIKIANO KATIKA KUTOA USHAHIDI JUU YA WATOTO

 

Ipo haja kwa wazazi na walezi kua na ushirikiano katika kutoa ushahidi juu ya watoto wao na kuachana na tabia ya muhali hali ambayo inazidisha udhalilishaji wa kijiinsia na kupelekea kuengezeka kwa vitendo hivyo.

Akizungumza na zbc mkuu wa wilaya ya mjini mhe.marina joel thomasa lipofika kumtembea mtoto huyo hospitali ya mnazi mmoja mwenye umri wa miaka sita  ambae inasemekana amemdhalilishwa  na baba yake mdogo mwenye umri wa miaka ishirirni tukio ambalo limetokea wilaya ya kati .

Amesema vitendo hivi vimnekuwa vimekithiri ipo haja kwa serikali kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale wote ambao wanahusishwa na vitendo hivi vya udhalilishaji.

Naye afisa kutoka tamwa bibi greace amesema serikali ifike wakati ichukuwe hatua za haraka za kuwaadhibu watu kama hao wanaofanya vitendo hivyo kwa makusudi kwani siku hadi siku vimekuwa vikiendelea katika jamii.