IPO HAJA YA KUBADILISHA KANUNI NA SHERIA ZA ADHABU KWA WAMILIKI WA HOSPITALI BINAFSI

 

Bodi ya ukaguzi wa hospatali  binafsi imesema  ipo haja ya kubadilisha kanuni na sheria  na vipengele vya adhabu kwa wamiliki wa  hospatali binafsi kwani imeonekana  hosptali hizo  zikileta  zarau kwa bodi hiyo  pale wanapopewa  masharti ya kurekebisha kasoro za kiuendeshaji  kutoyatimiza     na bodi hiyo  kukuta makosa  yakijirejea  wakati tayari  bodi hiyo imeshazikagua  hospatali hizo .Akizungumza na zbc mara baada ya kumaliza kwa zoezi hilo la kuzikagua hosptali hizo binafsi za wilaya ya magharib  b ambapo kati ya hosptali tano zilizofanyiwa ukaguzi na mbili kufungiwa hadi kukamilisha  masharti waliyopewa  msaidizi mrajisi wa ukaguzi wa bodi hiyo  khamis makame haji amesema  hali hiyo  imekuwa ikirudisha nyuma jitihada za bodi hiyo ambayo  inafanya kazi kisheria .

Aidha amewataka wamiliki hao kubadilika kwa kuzifuatilia  hospatali zao kwa kusimamia vyema   wanaowapa dhamana za kuziendesha hosptali hizo kwani mapungufu mengi ambayo kila bodi inapofanya ukaguzi ni tatizo la leseni zaufanyaji kazi kwa daktari na nasi  pamoja na muundo mzima wa uendeshaji hauko vizuri kwa baadhi ya sehemu . Hata hivyo katika hatua nyengine khamis amewataka  madokta kujenga utamaduni wa kupeleka tarifa za magonjwa mbalimbali za kila mwezi kwa afisi za afya za willaya DHMTambazo  zimekuwa zikikosa tarifa sahihi za maradhi ziliopo. Nae daktari dhamana wa j/m iliopo mpendae amesema zoezi hilo ni zuri kwani liwapan fursa ya kuondokana  na kufanya kazi kimazoea  na kuleta ufanisi wa kazi zao kwani  afya ya binadamu  inapotolewa lazima kuhakikishe  usalama wa tiba.  Bodi hiyo itazikagua  hosptali 20 zilizomo ndani ya mkoa wa mjini katika zoezi lake la ukaguzi ikiwa ni awamu ya pili kwa mwaka huu  ambapo katika  zoezi hili la leo imeifungia   Mustafa unal clin ya kisauni na  mji mpya dispensary  pamoja na Mombasa medical  centre sehemu ya kungoa meno