IRAN IMEKANUSHA MADAI KUUNGA MKONO WAASI NA KUZUIA JUHUDI ZA AMANI YEMEN.

 

 

Iran imekanusha madai yanayotolewa na saudi arabia kwamba nchi hiyo inaunga mkono waasi na kuzuia juhudi za amani nchini yemen.

msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya iran amesema nchi yake inalaani matumizi ya nguvu dhidi ya yemen tangu mwanzo na haitosita kuzuia juhudi zozote za kumaliza umwagikaji wa damu na vita visivyokubalika.

Saudi arabia inaongoza muungano wa kijeshi unaoiunga mkono serikali ya yemen katika mapambano dhidi ya waasi wa kishia wa kihuthi.

Pande zote zinazohusika katika mgogoro wa yemen zimekosolewa kwa kupuuza usalama wa raia lakini muungano wa kijeshi ukiongozwa na saudi arabia  umeshutumiwa kwa kushambulia kwa mabomu skuli,masoko na hospitali nchini yemen.