IRAQ KUANZISHA OPERESHENI YA KUUREJESHA MJI WA TAL AFAR

 

 

Waziri mkuu wa iraq haider al-abad amesema wamenzisha operesheni ya kuurejesha mji wa tal afar ulioko magharibi mwa mosul kutoka kwa kundi la is.

Tal afar ni miongoni mwa maeneo ya mwisho yanayodhibitiwa na is tangu mwaka 2014 nchini iraq baada ya serikali kutangaza ushindi katika mji wa pili kwa ukubwa wa mosul mwezi uliopita.

Waziri mkuu al-abad ameahidi kuukomboa mji huo wa tal afar ambao baadhi ya raia wameukimbia mji huo kama ilivyokombolewa miji mingine.

 

Wanamgambo wa kishia wamesema watashiriki kwa kiasi kikubwa kuukomboa mji wa tal afar ambao ulikuwa makazi ya wasunni na washia kabla ya kuangukia mikononi mwa is.