IS YAHARIBU MSIKITI MKUU WA MOSUL NA MNARA ULIODUMU MIAKA 840

Is yaharibu Msikiti mkuu wa Mosul na mnara uliodumu miaka 840

wanamgambo wa kundi la dola la kiislamu is wameuharibu msikiti mkuu wa Mosul wa Al-nuri na mnara wake maarufu ujulikanao kama Al-Hadba.

waziri mkuu wa Iraq Haider al-abadi amesema kuharibiwa kwa msikiti huo, kunadhihirisha kushindwa kwa wanamgambo katika vita vya kuukomboa mji wa mosul ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo.

is inadai jeshi la marekani limefanya shambulizi la angani lililouharibu msikiti huo wa kihistoria, madai ambayo yamekanushwa na Marekani.

wakati huohuo, umoja wa mataifa unaonya Is inawatumia watoto Mosul kama ngao kuwazuia raia kuukimbia mji huo.