ISMAIL OULD SHEIKH AHMED ATAJIUZULU MWEZI UJAO

 

Mjumbe wa umoja wa mataifa nchini yemen ismail ould sheikh ahmed atajiuzulu mwezi ujao wadhifa wake wa kuwa mpatanishi mkuu katika taifa hilo linalokumbwa na vita.

Taarifa iliyotolewa na umoja wa mataifa haikumtaja mrithi wa cheikh ahmed ambaye ni mwanadiplomasia wa mauritania, ambaye aliteuliwa kuwa mjumbe maalum kwa ajili ya yemen mnamo aprili 2015.

Licha ya majaribio kadhaa, umoja wa mataifa umeshindwa kuzishawishi pande zinazozozana kujiunga katika mazungumzo ya kutafuta suluhisho la kisiasa la kuumaliza mzozo wa nchi hiyo tangu ulipozuka mwaka wa 2014.

Zaidi ya watu elfu 15 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa tangu mwaka  2015, wakati saudi arabia ilipozindua operesheni ya kijeshi na wahouthi na washirika wao katika jaribio la kuiunga mkono serikali inayotambulika kimataifa ya rais wa yemen abed rabbo mansour hadi.