ISRAEL IMEANZA KUWAPATIA BARUA ZINAZOWAPA MUDA WA KUONDOKA NCHINI HUMO WAAFRIKA WANAOOMBA HIFADHI

 

 

Israel imeanza kuwapatia barua zinazowapa muda wa miezi miwili kuondoka nchini humo waafrika wanaoomba hifadhi na kuwataka kwenda katika nchi nyingine ambayo hawakuitaja.

Barua hizo zinaeleza kuwa waomba hifadhi hao wa kiafrika wapatao elfu 20 watapatiwa tiketi ya ndege pamoja na dola 3,500 kila mmoja.Mamlaka ya uhamiaji nchini israel imesema kuwa taarifa hizo zimepelekwa kwa wanaume ambao hawajaoa, wengi wao wakitokea eritrea na sudan.

Mamlaka hiyo imeonya kuwa wale wanaotakiwa kuondoka wamepewa hadi mwezi machi kuondoka la sivyo watafungwa gerezani na baadaye kufukuzwa.Mpango wa kuwapeleka wahamiaji hao kwenye nchi ya afrika ambayo haikutajwa, chini ya makubaliano ya siri, ulitangazwa januari 3 na waziri mkuu wa israel, benjamin netanyahu.