JAJI MKUU AMEWASISITIZA MAJAJI, MAHAKIMU KUHARAKISHA KUMALIZA KESI KWA WAKATI

 

 

Jaji mkuu wa zanzibar mhe, omar  othman makungu amewasisitiza majaji, mahakimu na  makadhi  kuharakisha kumaliza kesi kwa wakati ili wananchi kuendelea kuwa na imani na mahakama.Mhe, makungu amesisitiza hayo katika mkutano mkuu wa jumuiya ya majaji, mahakimu, makadhi na warajis wa mahakamauliofanyikamaruhubi.
Amesema ameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na watendaji hao hasa katika kupambana na kesi za udhalilishaji wa kijinsia na dawa za kulevya  ambazo ni janga la taifa.

Nae  katibu mkuu  wa jumuiya hiyo luciano makoye  amesema katika kipindi kilichopita jumuiya imeiomba idara ya mahakama kuiunga mkono katika mikutano ya kimataifa.
Aidha bw. Makoye amesema  katika mazimio yao wameahidi  kumaliza kesi za udhalilishaji wa kijinsia na dawa za kulevya.
Katika mkutano huo  hakimu salum hassan bakar amechaguliwa kuwa rais wa zajoa, jaji aziza iddi suweid kuwa makamo na luciano makoye  kwa  katibu muu.