JAJI MKUU ATISHIWA KIFO MALDIVES

 

Jaji mkuu wa maldives amepokea vitisho vya kuuwawa kabla ya kukamatwa katika msako wa serikali ya nchi hiyo, amesema wakili wake leo kabla ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzungumzia kuhusu mzozo wa kisiasa wa taifa hilo.

Jaji mkuu abdulla saeed alionywa kwamba atakatwakatwa vipande, iwapo hatabadilisha uamuzi wa mahakama wa kufuta hukumu dhidi ya wapinzani maarufu wa kisiasa.

saeed alikamatwa wakati rais abdulla yameen alipotangaza amri ya hali ya hatari katika kisiwa hicho baada ya kukataa kutii amri ya mahakama.

jaji huyo alishutumiwa kwa kupokea rushwa ili kumshitaki bungeni kiongozi wa nchi, ambaye amewafunga jela  wapinzani wake wa kisiasa.