JAJI MKUU MSTAAFU HAMID MAHMOUD HAMID KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (ZEC)

 

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk. Ali Mohamed Shein  amemuapisha Jaji mkuu mstaafu wa zanzibar hamid mahmoud hamid kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar (zec) pamoja na wajumbe wake sita aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya kuapishwa imefanyika ikulu mjini zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo makamu wa pili wa rais balozi seif ali idd, spika wa baraza la wawakilishi zubeir ali maulid, jaji mkuu wa zanzibar  omar othman makungu, mwanasheria mkuu wa zanzibar said hassan said, mawaziri pamoja na katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi dk. Abdulhamid yahya mzee na viongzi wengine wa dini.

Pamoja na jaji mkuu staafu hamid mahmoud hamid, wajumbe walioapishwa ni nd. Mabruki jabu makame, feteh saad mgeni, makame juma pandu, dk. Kombo khamis hassan, jaji khamis ramadhan abdalla na jokha khamis makame.

Mara baada ya kuapishwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar (zec) hamid mahmoud na wajumbe wake hamid ameahidi kutumia uzoefu alikuwa nao katika masuala ya uchaguzi kwa muda wa miaka saba akiwa makamo mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi (nec) huku wajumbewakiahidi kutekeleza majukumu yao kwa kufuata katiba, sheria na kanuni za tume na kuwaomba wazanzibari wote kutoa ushirikiano.

Nae

Nao viongozi wa vyama vya siasa wamempongeza rais dk. Shein kwa kuheshimu katiba ya zanzibar na kukidhi matakwa ya katiba hiyo ya mwaka 1984 ambayo inataka miongoni mwa wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi wawe ni kutoka vyama vya upinzani.

Kuteuliwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar (zec) pamoja na wajumbe hao kumekuja baada ya tume iliyopita kumaliza muda wao chini ya mwenyekiti wake jecha salim jecha ambao walifanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano.