JAMII IMESHARIWA KUJENGA TABIA YA KUPANDA NA KUTUNZA MIKOKO

 

Jamii imeshariwa kujenga  tabia ya kupanda na kuzitunza mikoko iliopo ili kuweza kutunza masalio ya samaki na mazingira ya ukanda wa bahari na kukabiliana na mabadiliko ya tabiayanchi.

Hatua hiyo itasaidia kuepuka  kupotea uoto wa asili katika ukanda wa pwani ambao ni muhimu kwa viumbe wa baharini na wattumiaji wa rasilimali hiyo.

Akizungumza wakati wa upandaji miti ya mikoko katika huko kisakasaka, naibu katibu wa jumuiya ya upandaji na uhifadhi wa mikoko kisakasaka (jumkisa) ndugu iddi hassan ali amesema koko zimekuwa zikiathirika na kupoteza uhalisia wake kutokana na jamii kuzikata ovyo na kutopanda mingine.

Amesema katika kukabiliana na upotevu wa koko  amesema wanakabiliana na changamoto kubwa  kutokana na jamii wakiwemo wakulima na wafugaji kukata kwa ajili ya kuhuwisha vipando vyao..

Akiongoza zoezi la upandaji mikoko mkurugenzi manispaa magharibi b amour ali amesema manispaa yake itashirikiana na wanajumuiya hao kwa ajili ya kupanda na kuitunza mikoko ili kurudisha uoto wa asili.

Zaidi ya miche 5000 ya aina tofauti ya mikoko imepandwa katika eneo la koko ya kisakasaka.