JAMII IMESISITIZWA KUWA KARIBU NA WATU WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Jamii imesisitizwa kuwa karibu na watu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo katika kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi.
Mbunge wa jimbo la chumbuni ussi salum pondeza amesema makundi hayo yamekuwa na mahitaji mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa kwa pamoja hivyo kupitia pondeza foundation atahakikisha jukumu hilo linafanikiwa.
Akizungumza katika chakula alichowaandalia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu mh. Pondeza amesisitiza umoja miongoni mwa jamii katika masuala muhimu ili kukuza ustawi wa jamii nzima.
Tukio hilo lilifuatiwa na kisomo maalum kutoka madrasa mbalimbali za jimbo hilo pamoja na wageni wengine.