JAMII IMETAKIWA KUFIKISHA MALALAMIKO YAO SEHEMU STAHIKI

 

Mkuu  wa  mkoa  wa kusini  unguja hassan  khatibu  amesema serikali  haina  dini  wala  haibagui  wananchi  wake  hivyo  amewataka jamii ya wakiristo  kuyafikisha  malalamiko  yao sehemu  stahiki  ili  yaweze kufanyiwa  kazi.

Akizungumza  na  madhehebu mbali  mbali  ya  dini  ya  kikristo kwenye kikao maalum mkuu huyo wa mkoa amesema serikali imeweka  viongozi kupokea  malalamiko  ya  wananchi kwa vile kila  mwananchi ana  nafasi  sawa  katika kupata  haki  zake za msingi.

Mkuu  wa  wilaya ya mjini marina  joel  thomas  amesema wananchi kwa ujumla wake wanapawa kuongeza ushirikiano na kuunda  kamati  zitakazoongeza  kasi  ya  mapambano  dhidi  ya  vitendo  vya  udhalilishaji  vinavyojitokeza  ili  kuweza  kudumisha  amani  iliopo  nchini.

Kwa  upande  wao  viongozi  na  waumini  wa  dini  ya  kikristu  wameomba kupatiwa   nafasi  ya  kusomesha elimu  ya  dini yao  katika  skuli pamoja na kupatiwa  hakimiliki  ya  maeneo  yao  ya  makanisa.

Kikao  hicho  cha  siku  moja  kilichoandaliwa  na  kamati  tekelezaji  ya  mkoa  kusini  unguja kimewashirikisha  viongozi  na  waumini  wa  madhehebu  ya dini  ya  kikristu wa  wilaya  ya  kati.