JAMII IMETAKIWA KUPANDA MITI MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA UCHIMBAJI MCHANGA ILI.

 

jamii imetakiwa kuhamasishana kupanda miti maeneo

yaliyoathirika kwa uchimbaji mchanga ili

kuyarejeshea uhalisia wake na kuepuka

mmong’onyoko wa ardhi.

mkuu wa kitengo cha  maliasili  zisizorejesheka idara  ya  misitu ngwali  makame  haji akizungumza katika  upandaji  miti   mangapwani na fujoni amesema maeneo hayo yanaweza kutumika tena iwapo yatapandwa miti upya.

sheha wa shehia wa mangapwani  nd.  Folabasb  Maridadi  amesisitiza wamiliki wa maeneo yaliochimbwa mchanga  wanapomaliza shughuli zao kupanda  miti  ili kutumika kwa kilimo.

wananchi  wa  vijiji  hivyo wameahidi  kushiriana kulifanya  zoezi la upandaji miti kuwa endelevu kwa faida yao pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira.