JAMII KUWA NA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA KABLA YA KUSUBIRI KUUGUA

Waziri wa afya mh.mahmoud thabit kombo ameiomba jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya kabla ya kusubiri kuugua kwani itasaidia kujua afya zao mapema.
Mh. Mahmoud ametoa kauli hiyo wakati alipokagua kambi ya matibabu ya macho inayoendelea katika skuli ya kiembe samaki ambayo inaendeshwa na madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo sweden na canada.
Aidha waziri mahmoud amesema wizara ya afya imekuwa ikiandaa utaratibu wa kuleta madaktari bingwa wa kusaidia jamii kwa kushirikiana na mashirika ya kimaendeleo kila baada ya muda kwa lengo la kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi kufuatia maradhi mbalimbali yakiwemo ya macho na kuwataka kuitumia ipasavyo fursa hiyo.
Nae mratibu wa huduma za macho vijijini dr. Rajab mohammed amesema muendelezo wa kuwapatia huduma wananchi unaoendeshwa na taasisi ya spect savers ambayo ipo kwa siku nne, imefanya huduma hizo kwa awamu sita na imesaidia zaidi ya watu elfu nne kila awamu.