JAMII KUWA NA UTARATIBU MZURI WA UEZEKAJI WA NYUMBA ZAO ILI KUEPUKANA NA MAJANGA YA UPEPO

Mkuu wa wilaya ya kaskazini b issa juma ali ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu mzuri wa uezekeji wa nyumba zao ili kuepukana na majanga ya upepo pamoja na mvua
Wito huo ameutoa katika ziara ya kuwatembelea wahanga walioezuliwa mabati nyumba zao kwa upepo uliojitokeza hafla huko mahonda minanasini
Mkuu wa wilaya ya kaskazini b issa juma ali amesema matukio mengi ya kuezuka kwa nyumba yanatokana na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa uezekaji kitendo ambacho kinapelekea maafa hasa katika kipindi cha mvua na upepo
Amesema maeneo mengi ya kisiwa cha zanzibar ni maeneo tambarare hivyo ni vyema jamii ikawa makini katika uezekaji wa nyumba zao ili kujiwekea uhakika wa kujikinga na maafa hasa yale ya upepo na mvua
Fatma juma ali na sabra muhammedi ni miongoni mwa wahanga ambao nyumba zao zimeezuliwa kwa upepo uliovuma hafla katika maeneo ya mahonda minanasini licha ya kutokuwepo kwa hasara kubwa kwa wahanga hao
Nyumba tatu zimeezuliwa mabati kufuatia upepo mkali uliovuma majira ya saa saba mchana wa jana na hakuna mtu yoyoyte aliyejeruhiwa