JAMII KUWASAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA KWA SHUGHULI MBALI MBAL

 

Jamii imetakiwa kuwasaidia wazee wasiojiweza kwa shughuli mbali mbali ikiwemo usafi ili nao wajione na thamani kwenye jamii kama watu wengine.Akizungumza  katika zoezi la usafi kwenye nyumba za wazee welezo katika kusheherekea muungano wa tanganyika na zanzibar mkuu wa mtandao wa wanawake wa jeshi la polisi mkoa wa mjini magharibi  asp akama mohd shaabani amesema baada ya kujua umuhimu wa wazee wameona kuna haja ya kwenda kuwasafishia kwenye nyumba zao

Amesema ikiwa leo ni siku ya muungano wa tanganyika na zanzibar wameona ipo haja ya kukaa pamoja na wazee hao kwani wananafasi kubwa sana katika nchi yao ya tanzania.

Nae sister rita kabiru ambae ni kiongozi kwenye nyumba hizo za wazee welezo amesema wamefarijika sana kuona jeshi la polisi linawasaidia wazee hao huku akiwaomba watu wengine kujitokeza kuwasaidia wazee hao.

Nao baadhi ya wanachama wa mtandao wa wanawake wa jeshi la polisi mkoa wa mjini magharibi afande zainab ali na catherine boniphace wamezungumzia zoezi hilo lilivyokwenda huku wakiwaomba wananchi mbali mbali kuwasaidia wazee hao.