JAMII NCHINI IMETAKIWA KUZINGATIA UTABIRI UNAOTOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

 

Jamii nchini imetakiwa kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ili kuepuka athari  za upepo na mvua kubwa. mkurugenzi  mtendaji  kamisheni  ya kukabiliana  na  maafa  makame khatib makame ameleza hayo katika kijiji cha chwaka akiwa  katika ziara maalum ya kukagua na kuwapa pole wananchi walioathiriwa na upepo uliosababisha nyumba zao kuezuka mapaa.Aidha  amesema kuna haja kwa jamii kuchana na tabia ya kuezeka kwa kulaza mabati  kwani hali hiyo haistahamili misukosuko ya upepo unapovuma hasa katika maeneo yalio karibu na ukanda wa bahari.Nae sheha wa shehia ya chwaka bwana simai msaraka  pinja ameleza kuwa upepo uliovuma umepelekea athari kwa zaidi ya nyumba kumi kuezuka mapaa pamoja na soko kubwa la kuuzia samaki .Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha chwaka bwana maulid abasi ameiyomba serikali kutoa msaada kwa wananchi waliopatwa na athari ya upepo ili kurejesha hali kwa kupata sehemu za kujistiri na familia zao.