JAMII YATAKIWA KUJIUNGA NA VIKUNDI MBALIMBALI VYA MICHEZO

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini  b  rajab ali rajab ameitaka jamii kujiunga katika vikundi mbalimbali vya michezo ili kuimarisha afya, kujikinga na maradhi mbalili,  pamoja na kudumisha umoja na mshikamano

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kushiri bonanza la clinic ya mazoezi lililofanyika  katika  uwanja  wa skuli ya  bum bwini makoba

Akizungumza   na wananchi, wanakikundi cha  new   life execise,pamoja na wanachama wa chama cha mpira  wa mikono  zanzibar    ndugu rajab amesema mazoezi yanafaida kubwa kwa jamii ikiwemo  kuunganisha umoja wa mshikamano pamoja na kumkinga  mtu na vitendo  viovu  ikiwemo udhalilishaji

Kwa upande wake  katibu wa kikundi   cha mazoezi new life exercise ndugu nasir salum buheti amesema  kikundi hicho kimeamua kwenda kufanya bonanza la clinic  katika wialaya hiyo ili kuhamasisha jamii hiyo kuwa na desturi ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao

Sheha wa shehiya ya bumbwini makoba juma zahor juma amesema kupitia bonanza hilo atahakikisha anaihamasisha jamii ya watu wa bumbwini kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Wakati huohuo mkuu wa wilaya ya kaskazini b rajab ali rajab amezindua kalenda ya chama cha mpira wa wavu  na kukabidhi kalenda hizo kwa skuli mbalimbali zilizoshiriki mchezo huo uliofanyika katika pwani ya kiwengwa