JAMII YATAKIWA KUWATHAMINI NA KUJENGA UPENDO KWA WATOTO YATIMA

 

 

Jamii imetakiwa kuwathamini na kujenga upendo  watoto yatima ili waweze kuishi katika mazingira  bora, kwa kuwapatia elimu na huduma nyengine muhimu za kijamii.

Akishiriki katika kazi ya usafi kwenye nyumba ya kulelea watoto yatima iliyopo mazizini naibu katibu mkuu jumuiya ya muzdafah, othman muhamed saleh akiongozana na watoto yatima wanaolelewa na jumuiya hiyo amesema watoto yatima ni sawa na wengine kwani wanamchango mkubwa wakuleta maendeleo ya kijamii na kitaifa, hivyo ni vyema wazazi na jamii kuona umuhimu wa kuwatunza na kuwatendea mambo yaliyo mema.

mlezi mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima mazizini bi saida ali muhamed,ameelezea kuridhishwa na hatua hiyo ya jumuiya ya muzdalifah kufanya usafi katika nyumba hiyo na kuiomba jamii kuwacha tabia ya kuwatupa watoto kwa kisingizio cha kushindwa kuwalewa kutokana na hali ngumu ya maisha

baadhi ya watoto yatima wanaotunzwa na jumuiya ya muzdalifah wamesema ushiriki wao umelenga kuwajali wenzao

Kazi hiyo ya usafi ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya yatima, itakayofikia kilele chake tarehe nane mwezi huu katika kijiji cha fumba.