JAMIII IMETAKIWA KUWALINDA WARI NA WAJANE ILI KUWAEPUSHA NA VISHAWISHISHI VITAKAVYOPELEKEA KUPATA UJAUZITO

Jamiii imetakiwa kuwalinda wari na wajane ili kuwaepusha na vishawishishi vitakavyopelekea kupata ujauzito na kusababisha watoto watakaozaliwa kukosa malezi bora kitoka kwa wazazi wake.
Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufahamu sheria ya kuwalinda watoto wari na wajane pamoja na mtoto wa mzazi mmoja afisa mipango wa kituo cha huduma za sheria zanzibar moza nzole amesema tathmini inaonesha kuwa watoto wengi wanakosa matunzo ya wazazi wawili kutokana na jamii kutoifahamu sheria hiyo.
Amefahamisha kuwa kuna baadhi ya akinanababa wanawakimbia na kuwatelekeza watoto wao kwa kuona kuwa watoto hao sio wa kwake
Aidha amesema mafunzo hayo yanalengo la kuwapa uelewa wa kujua jinsi gani ya kuweza kupambana na baadhi ya wanaume wa namna hiyo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kwa kiasi kikubwa wameweza kufahamu namna gani ya kumkomboa mtoto katika kupata malezi bora yatakayoshirikisha pande zote mbili pamoja na kuwadhibiti wari na wajane waondokane na vishawishi.

.