JESHI LA IRAQ LASHEREHEKEA USHINDI MOSUL

Wanajeshi wa iraq wakishirikiana na majeshi ya marekani wanasherehekea kuuomboa mji wa mosul uliokuwa ngome ya mwisho ya wapiganaji wa dola ya kiislamu is.
Mosul, mji wa pili kwa ukubwa, ulikuwa mikononi mwa is tangu mwaka 2014, na wamefanya mashambulizi kadhaa yaliyosababisha vifo vya maelfu ya raia na wengine kuukimbia mji huo.
Waziri mkuu haider al-abadi ameelezea kufurahishwa na hatua hiyo ingawa amesema bado kuna changamoto nyingi zinazikabili iraq.
Al-abadi ameutembelea mji wa mosul na kukutana na makamanda wake pamoja na raia