JESHI LA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO LIMEWAUWA WAASI 25

Jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya congo linasema limewauwa waasi 25 wa mai mai baada ya mapigano yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani beni.
Katika makabiliano hayo ya kudhibiti eneo la kabasha watu 13 kupoteza maisha, wakiwemo waasi wa mai mai 12 na mwanajeshi mmoja.
Wakati uo huo, kundi lisilofahamika la waasi linalojiita vuguvugu la kitaifa la mapinduzi mnr, linadai kuwa ndilo lililokabiliana na wanajeshi wa serikali, ambapo john mangaiko ameliambia shirika la habari la ufaransa kuwa wao ndio waliohusika na makabiliano hayo.