JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LINAKUSUDIA KUFANYA OPERESHENI

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linakusudia kufanya operesheni maalum ya kupambana na wahalifu na wanaouza vifaa vya  umeme vya wizi katika mkoa huo.

Oporesheni hiyo imekuja kufuatia kuibuka kwa wimbi la wizi wa vifaa hivyo unaofanywa na wahalifu wanaovunja nyumba jijini dar es salaam.

Tupate taarifa zaid.

Kaimu kamanda wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam lucas mkondya amebainisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wafanyabiashara wanaouza vitu vilivyotumika bila ya kuwa na stakabadhi kujisalimisha kabla hawajakamatwa kwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyengine kamanda mkondya amesema jumla ya watuhumiwa 275 wamekamatwa jijini dar es salaam kwa makosa mbalimbali ya kiharifu kuanzia julai 20 hadi august 3 mwaka huu.

Aidha amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kukamata silaha aina ya chinese pistol ikiwa na risasi moja iliyopatikana baada ya majambazi watatu waliokuwa kwenye pikipiki kupora pesa shilingi milioni 10 ,simu mbili na kompyuta mpakato moja na kukimbia