JESHI LA POLISI KUFANYA KAZI KWA UMAKINI KUPUNGUZA UHALIFU

 

Mkuu wa mkoa wa kusini unguja mhe hassan khatib hassan amelitaka jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuweza kupunguza vitendo vya uhalifu nchini.
Akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kamishna mpya wa polisi zanzibar  afisi kwake tunguu  ambae ameteuliwa hivi karibuni mkuu wa mkoa amesema wananchi wanahitaji kuishikwa kwa usalama hivyo poalisi wanapaswa kufanya kazi ya ziada ili kuona hakutokei matukio ya uhalifu.

Amesema ili kupunguza vitendo vya uhalifu nchini juhudi za jeshi la polisi zinahitajika kuelekezwa pamoja na mambo mengine katika kupambana dhidi ya utumiaji wa madawa za kulevya na rushwa.

Nae kamishna mpya wa polisi zanzibar moh’d hassan haji amesema jeshi la polisi nchini limejipanga vyema kutekeleza majukumu yake na kuwataka viongozi na wananchi  kumpa mashirikiano.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wameahidi kumpa mashirikiano ya kutosha kamishna huyo ili kuona hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaimarika