JESHI LA POLISI KUPUNGUZA AJALI NA KULINDA USALAMA WA WANANCHI

 

Mkuu wa trafik zanzibar ssp robert patric hussein amesema watahakikisha wanashirikiana na jeshi la polisi barabarani katika kupunguza ajali na kuninda usalama wa wananchi.

Akifungua semina ya usalama barabarani iliyowashirikisha walimu, wanafunzi, madereva na wazazi huko katika ukumbi wa skuli ya haile salasie, amesema takwimu inaonyesha kwa mwaka huu 2018 ajali zimepungua kwa asilimia 50 ukilinganisha na mwaka uliopita.

Amesema kupungua kwa ajali hizo zimetokana na mikakati yao ya kutoa elimu katika vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wamepata elimu na kupungua kwa ajali hizo.

Nae mkuu wa trafik wilaya ya mjini mohammed talhata kwa upande wake amewataka wanafunzi kuzitumia zebra ili wavuke barabara kirahisi na kuepukana na ajali za kizembe.

Kwa upande mratibu wa semina hiyo bwana nuru mtema  kutoka kituo cha vijana cha stone town youth center kupitia mradi wa tuna ndoto amesema lengo la kuandaa semina hiyo ni kumlinda kijana kutimiza ndoto zao.

Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwemo walimu na madereva wamesema kumalizika kwa mafunzo hayo itawasaidia kuisambaza elimu hiyo ili ajali zipunguwe.