JESHI LA POLISI LIMETAKIWA KUFANYA UCHUNGUZI KUFUATIA UHARIBIFU WA KUIBA MITA KATIKA KISIMA

Jeshi la polisi limetakiwa kufanya uchunguzi kufuatia uharibifu uliofanywa na baadhi ya watu waliokata nyaya za umeme na kuiba mita katika kisima cha maji cha shehia ya dimani.
Akikagua kisima hicho mkuu wa wilaya ya magharib ‘b’ silima haji amesema kitendo hicho kinarudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kulitaka jeshi hilo kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kuhusika na uharibifu huo
Aidha ameitaka mamlaka ya maji zanzibar zawa kurudisha huduma ya maji katika eneo hilo.ili kuwaondoshea usumbufu wananchi hao
Sheha wa shehia ya dimani khamis ame baraka amewataka wakaazi wa eneo hilo kutoa taarifa kwa uongozi wa shehia watakapowabaini watu waliofanya hujuma hiyo ili kufikishwa katika vyombo vya sheria
Kwa upande wake mrakibu wa polisi ramadhan hassan ameitaka serikali ya wilaya,ya magharibi b na mamlaka ya maji zanzibar zawa kuweka ulinzi katika eneo hilo ili kudhibiti hujuma hizo zisifanyike