JESHI LA POLISI WILAYA YA KUSINI LIMESEMA HALITOMVUMILIA ASKARI YOYOTE ATAKAEBAINIKA KUSHIRIKIANA NA WAHALIFU

 

Jeshi la polisi wilaya ya kusini limesema halitomvumilia askari yoyote atakaebainika kushirikiana na wahalifu au kutoa siri za jeshi hilo pale linapopangwa mikakati ya kazi za doria.

Mkuu wa polisi wilaya hiyo ocd, ali mselem ali ametoa onyo hilo wakati akijibu malalamiko ya wananchi wa shehia ya kijini makunduchi wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya kusini idrisa kitwana mustafa na kuhimiza askari wote wanatakiwa kutekeleza majuku yao kwa mujibu wa sheria na sivyenginevyo.

Ocd ali amewataka wananchi wasisite kutoa taarifa mbaya wanapobaini askari wanatumia  mwanvuli wa kazi yao kwa kujishirikisha katika  vitendo viovu.

Wananchi hao wamelalamika kuwa  baadhi ya askari wamekuwa wakishirikiana na wahalifu kwa kutoa  taarifa mbali mbali za jeshi hilo zikiwemo  za kufanya doria za kuimarisha ulinzi.

Mkuu wa wilaya ya kusini idrissa mustafa kitwana amesema wilaya yake imejipanga katika kupamabana na vitendo vya uhalifu  hivyo amewataka wazazi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kuwafichua wahalifu kwani wengi wao wamo katika familia zao.

Ziara ya mkuu huyo ni muendelezo wa kufika vijiji vyote vilivyomo katika wilaya hiyo kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.