JESHI LA POLISI ZANZIBAR LIMEZINDUA MASHINDANO YA LIGI YATAKAYOZISHIRIKISHA TIMU ZA POLISI WILAYA ZOTE

 

Jeshi la polisi zanzibar limezindua mashindano ya ligi yatakayozishirikisha timu za polisi wilaya zote za unguja na pemba na kutakiwa kuendeleza nidhamu katika mashindano hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho atakapopatikana bingwa.

Katika mashindano hayo katibu na mwenyekiti wa mashindano  kibabu na mkadam khamis wamesema nia na lengo ni kuendeleza michezo yote na kukuza vipaji vya michezo.

Kamishna wa polisi  hamdan omar amesema ni muhimu jeshi la polisi kuonyesha vipaji vyao ambavyo vitahitaji kutunza kwa lengo la kushiriki michezo mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Awali rais wa zfa  na mwenyekiti wa baraza la michezo waliahidi kuchangia michezo hiyo.

Katika mchezo wa fungua dimba  polisi wilaya ya mjini iliifunga ffu  mjini kwa mabao  2 – 1