JESHI LA ZIMBABWE LIMECHUKUA MAMLAKA YA NCHI HIYO LICHA YA KUKANUSHA

 

Jeshi la Zimbabwe limechukua mamlaka ya nchi hiyo licha ya kukanusha kuwa hatua hiyo haikuwa ni mapinduzi ya kijeshi.

Asubuhi ya leo ilikuwa bado haijafahamika wazi aliko rais wa nchi hiyo robert mugabe huku kukiwa na habari kuwa kiongozi huyo anashikiliwa na jeshi.

Msemaji wa jeshi la nchi hiyo sibusiso moyo amesema  kuwa mugabe na familia yake wako salama na wamehakikishiwa usalama wao.

Amesema anataka ifahamike wazi kuwa hatua hiyo hailengi jeshi kuchukua madaraka ya serikali bali jeshi lilikuwa linawalenga wahalifu wanaomzunguka kiongozi huyo ambao wanadaiwa kusababisha matatizo ya kiuchumi.

Moyo amesema mara tu watakapokuwa wamekamilisha operesheni yao wanatarajia kuwa hali itarejea kuwa kama kawaida.

Hali haikuwa shwari katika mji mkuu wa nchi hiyo harare  asubuhi ya leo  wakati ofisi za Rais mugabe pamoja na bunge zikiwa zimezingirwa na vikosi vya usalama huku vifaru vikionekana kufanya doria katika mji huo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa jeshi limefanya mapinduzi licha ya kukanusha.