JICA KUWASAIDIA VIJANA WA TANZANIA MAFUNZO KATIKA SEKTA YA VIWANDA

Shirika la kimataifa la maendeleo la japani jica limesema litaendelea kuwasaidia vijana wa tanzania mafunzo katika sekta ya viwanda ili kufikia lengo la mabadiliko katika sekta hiyo.
Mpango huo wa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya uzamili yanatolewa kupitia mradi wa abe innitiative unaofadhiliwa na shirika hilo.
Hayo yameelezwa na rais wa shirika hilo shinichi kitaoka wakati akiwaaga vijana waliopata bahati ya kuhudhuria masomo hayo chini ya mpango wa abe initiative jijini dar es salaam kutoka tanzania bara na zanzibar na kuishukuru serikali ya tanzania kwa kuonesha ushirikiano kwenye miradi mbali mbali inayofadhiliwa na shirika hilo .
Nae balozi wa japani nchini tanzania mashaharu yoshida amesema matarajio yake ni kuona vijana hao wanaitumia fursa hiyo vizuri ili kufikia mafanikio yaliyokusudiwa ya kuwaandaa katika kukabiliana na sera ya tanzania ya viwanda ambapo sekta binafsi hutoa mchango mkubwa.
Nae mkurugenzi kutoka ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora laurean ndumbaro amewataka vijana hao kuitumia fursa hiyo kwa kusoma kwa bidii ili ujuzi watakao upata waweze kuutumia katika kuleta maendelea ya taifa lao.
Wakati huo huo kijana kutoka zanzibar ambae alibahatika kuwa miongozi mwa vijana hao kutoka sekta binafsi nd. Jalali dakhala ameir amesema amefurahi sana kuwa miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa na kuiomba serikali ya mapinduz i ya zanzibar kuwashajihisha vijana kutumia fursa za masomo zinazojitokeza kutoka nchi mbali mbali duniani kwa lengo la kupata ujuzi ambao utasaidia kuleta maendeleo nchini.