JIMBO LA MAKUNDUCHI KUTEKELEZA MIRADI 8 YA MAENDELEO

Uongozi jimbo la makunduchi unatarajiwa kutekeleza miradi 8 ya maendeleo ikiwa ni juhudi za kuondoa kero kwa wananchi wa jimbo hilo katika kipindi cha mwaka 2017-2018.
Akizungumza katika kikao cha utekelezaji mwakilishi wa jimbo hilo mh haroun ali suleiman amesema miradi hiyo ni pamoja na ya maji, elimu, na miundominu ya usafiri itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 24.
Amewaomba viongozi wanaosimamia miradi hiyo kuwa waaminifu ili kufikia lengo la kutatua kero katika jamii.
Katibu wa kamati ya maendeleo ya jimbo la makunduchi kasim mtule amesema miradi hiyo imeridhiwa na wananchi kwa kufuata demokrasia na imepitishwa na shehia kwa mujibu wa matatizo yanayowakabili