JITIHADA KUHAKIKISHA SERIKALI INAKOMESHA MATUMIZI NA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA

 

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Muhamed aboud muhamed amesema jitihada zinaendelea  kuhakikisha serikali inakomesha matumizi  na usafirishaji wa dawa za kulevya ili kuondoa uwezekano wa vijana kupata madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo.

Akizungumza  katika  madhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za ulevya duniani yaliyofaniyika katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu ya mapinduzi muembe kisonge michenzani mhe, aboud amesema  serikali ikishirikiana na serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania  zimedhamiria  kuhakikisha uzaji na usambazaji wa dawa  za kulevya  unaisha hapa nchini.

Amewaasa vijana wa zanzibar wanaofanya kazi katika meli za kigeni kuacha kujishughulisha na usafirishaji wa dawa hizo kwani hivi sasa kumekuwa na lawama za kujiingiza na usafirishaji wa dawa za kulevya jambo linloitia sifa mbaya zanzibar na kuvitaka vyombo vya usalama kuacha kushirikiana nawahalifu wa dawa za kulevya.

Mkuu wa mkoa wa mjini magharib mh muhamed ayoub amewaoma  mawakili wanaosimamia kesi  za madawa ya kulevya kuacha kuwachukuliwa dhamana watu wanaokamatwa na dawa hizo kwa kiwango kikubwa ili kukomesha kuendelea na biashara hizo.

Ndgu sleima maulid ambae alikuwa akitumia dawa hizo na baadae kuamua kuacha ameeleza jinsi alivyojiingiza kwenye dawa za kulevya na kisha kuziacha moja kwa moja.