JITIHADA ZA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

 

 

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar inaendelea  na jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikumba dunia hususan katika sekta ya kilimo.

Hatua hio ya serikali imebainishwa na makamu wa pili wa raisi wa zanzibar balozi seif ali iddi   wakati akizungumza na ujumbe wa maofisa na wataalamu wa kilimo kutoka korea kusini aliokutana nao ofisini kwake jijini dar es salam.

Mh. Balozi seif aliwaeleza wataalamu hao kuwa serikali imeamua kutafuta mbinu mbadala ya kuendeleza shughuli za kilimo kupitia kilimo cha umwagiliaji kutokana na mvua za misimu kuaathiri mtiririko wa shughuli hizo kufuatia mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, makamu wa pili amebainisha suala la ukusanyaji wa maji ya mvua, na kuyatumia kwa shughuli za kilimo, badala ya kuyawacha yanapotea.

Kwa upande wao maofisa hao walimweleza makamu wa pili wa raisi wa zanzibar kuwa msingi wa maendeleo yaliyofikiwa na jamii ya wananchi wa vijiji vya  korea kusini ni teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji. Mwisho…