JITIHADA ZA KUWAENDELEZA NA KUWAINUA KIUCHUMI WAJASIRIAMALI

 

Katika jitihada za kuwaendeleza na kuwainua kiuchumi wajasiriamali, mbunge wa jimbo la uzini mh salum rehani ameanza kuwawekea mitambo maalum kwa ajili ya kusindika maziwa.

Hatua hiyo itaweza kuwasaidia wajasiriamali hao kuwainua kutokana na hali duni ya kimaisha.

Pamoja na hali hiyo mbunge huyo amewapelekea wajasiriamali hao wajumbe kutoka benki ya taifa ya biashara nbc ili kuwaelimisha na kuweza kupatiwa mikopo nafuu ili kuendeleza shughuli zao.

Akizungumza baada ya mkutano kati ya wajasiriamali hao mh. Rehani  amesema bado wajasiriamali hao wanahitaji kupatiwa mikopo ili waweze kukuza mitaji yao.

Nao baadhi ya wajasiriamali hao wamesema uwepo wa benki ya nbc utawasaidia kupata mikopo na kuweza kukuza mitaji yao na kujikwamua na umasikini, huku wakimpongeza mbunge wao kwa juhudi anazozichukua katika kuwainua wajasiriamali hao.

Nae meneja wa benki ya nbc tawi la shangani bw ramadhan lesso amewapongeza wajasiriamali hao kwa kuweza kujikusanya na kuzalisha bidhaa mbalimbali  ambazo ndio zinazochangia kujiinua kimaisha.

Wajasiriamali hao wamekuwa wakijishughulisha na ufugaji wa ngombe, kilimo, kusindindika maziwa pamoja na shughuli mbalimbali.