JITIHADA ZA VISIWA VYA COMORO KUTAKA KUJIUNGA NA (SADC).

 

Serikali ya Tanzania imeunga mkono jitihada za Visiwa vya Comoro kutaka kujiunga na (SADC).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 3 March 2017 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Comoro hapa nchini Dkt Ahamada El Badaoui Mohamed Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inaunga mkono jitihada hizo za nchi ya Comoro kujiunga na SADC kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa nchi hiyo na kwamba tathmini iliyofanywa na Sekretarieti ya SADC  imeonyesha kuwa nchi hiyo inakidhi vigezo vya kupewa uanachama.

 Kwa upande wake, Balozi wa Comoro hapa nchini Dkt Ahamada El Badaoui Mohamed Ikulu Jijini Dar es Salaam imeishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya kuisaidia Comoro hasa inapokubwa na machafuko. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Katarina Rangnitt ambaye ameunga mkono jitihada za serikali ya awamu wa Tano katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi kama hatua ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa viwango vinavyotakiwa kote nchini. Makamu wa Rais Mhe

Samia Suluhu Hassan amemweleza balozi huyo kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama ana jambo zuri na lenye manufaa kwa taifa au anakwazwa na jambo lolote basi afike ofisi kwake ili wajadiliane na kuona namna ya kutafutia ufumbuzi.