JITIHADA ZINAHITAJIKA KATIKA KUTOA ELIMU YA UJASIRIAMALI VIJIJINI

 

Bado jitihada zaidi zinahitajika katika kutoa elimu ya ujasiriamali vijijini ili iweze kusaidia katika kubuni miradi na kuweza kufanya biashara zenye utaalamu.

Wakitoa michango yao washiriki wa kongamano la ujasiriamali wamesema tatizo kubwa linalochangia wajasiriamali wengi hasa wa vijiji kushindwa kujiendeleza kutokana na kutopata mafunzo ya mara kwa mara.

Mkurugenzi idara ya mikopo kutoka wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto nd. Suleiman ali amesema licha ya idara kutoa mikopo bado kumeonekana na tatizo kubwa kwa upande wa wanawake kuchukua mikopo midogo midogo kuliko wanaume.

Nd. Suleiman amesema  hali hiyo inasababisha wanawake wengi kushindwa kukua kiuchumi na kutoendelea mbele katika miradi yao.