JUHUDI ZA KUTAKA KUUNDA SERIKALI YA MSETO WA VYAMA VITATU ZIMEGONGA MWAMBA.

 

Kansela wa ujerumani angela merkel amesema juhudi za kutaka kuunda serikali ya mseto wa vyama vitatu zimegonga mwamba.

Hatua hiyo sasa imeitumbukiza ujerumani katika mgogoro wa kisiasa na kuipeleka katika uwezekano mkubwa wa kufanyika uchaguzi mpya.

Chama cha kiliberali cha wanaopendelea biashara cha free democrats fdp kilijitowa ghafla kwenye mazungumzo yaliyofanyika mfululizo kwa kipindi cha wiki nne na muungano wa kihafidhina unaoongozwa na kansela merkel pamoja na chama cha kijani.

Kiongozi wa chama cha fdp amedai kwamba wamejitowa kutokana na kuwepo tafauti zisizoweza kumalizwa kuhusu masuala muhimu.

Kansela merkel amesema ataendelea kukaimu nafasi hiyo na atashauriana na rais wa shirikisho frank walter-steinmeier kuhusu hatua itakayofuata.