JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUTIMIZA AHADI ZAKE

 

Wananchi wa ngomeni shehia ya mgelema wamesifu juhudi za serikali katika kutimiza ahadi zake za kupelekea maendeleo katika shehia hiyo ambazo zimepunguza kero mbalimbali.

Wananchi hao w3ameyasema hayo wakati walipotembelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar huko mgelema ikiwa ni ziara ya kuangalia miradi mbalimbali ya maendeleo katika shehiy

Wamesema kwa muda mrefu kijiji chao  kilikosa huduma muhimu ambapo kwa sasa huduma hizo zinapatikana ikiwemo huduma ya maji safi na salama

Mapema akizungumza na wananchi hao mkuu wa mkoa wa kusini pemba mh mwanajuma majid abdalla amewataka wananchi hao kuthamini huduma   za serikali na kuzitunza kwa maslahi yao na kizazi kijacho

Naye waziri asiyekuwa na wizara maalum mh juma ali khatib ameitaka wizara ya afya kufanya bidii katika kumaliza kituo hicho ili lengo lilikusudiwa  liweze  kufikiwa.