JUHUDI ZA SERIKALI KUWAPATIA ELIMU MBADALA WATOTO WALIOACHA SKULI KWA SABABU MBALI MBALI

Licha ya juhudi za serikali kuwapatia elimu mbadala

Watoto walioacha skuli kwa sababu mbali mbali

Baadhi ya wanafunzi hao bado hukimbia madarasani

Jambo linalowakatisha tamaa walimu

Wanaowasomesha.

Hayo yamethibitishwa na walimu wanaowasomesha watoto hao wakati walipopatiwa  mafunzo ya mbinu bora za kuwapatia elimu itakayowawezesha kujitegemea katika kuendesha maisha yao.

Mkuu wa divisheni ya idara ya elimu mbadala na watu wazima bibi halima tawakal khairalla  amesema lengo la kuwapatia walimu mafunzo hayo ni kutaka waweze kuwadhibiti wanafunzi wanaojiunga na madarasa hayo hasa kwa wanaoonekana kuwa ni wakorofi.

Mapema akifungua mafunzo hayo mkurugenzi wa idara hiyo nd.mashavu ahmada fakih amewataka walimu wanaosomesha madarasa ya elimu mbadala kutovunjika moyo katika kuwaendeleza watoto wanaorejea masomoni kwani mchango wao wa kuleta maendeleo unahitajika kwa taifa.