JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUPUNGUZA MATUMIZI MABAYA RASILIMALI

Serikali ya mkoa wa mjini magharibi imeanzisha operesheni mpya ya kukabiliana na uchimbaji wa mchanga na ukataji miti ili kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza matumizi mabaya rasilimali hizo.

Opereshani hiyo itaanzia na tatizo la uchimbaji mchanga kwa watatembelea vituo vya uchimbaji wa rasilimali hiyo na kupigia matofali ili kujiridhisha kama wamefuata taratibu za kisheri

Chanzo cha kikubwa cha uchambaji mchanga kinadaiwa ni  ongezeko la ujenzi holela hasa katika mkoa huo ambapo inakadiriwa kiasi ya hekta kumi na nne zimeshachimbwa mchanga.

Mkuu wa mkoa huo ayoub mahmoud amesema aidha pia imewataka wauza michanga kutoikusanya katika sehemu moja kabla ya kuuza kwani ni pia inachangia uharibifu wa mazingira.

Aidha mkoa huo umepiga marufuku matumizi na umiliki wa misumeno ya moto na kuwataka wenye misumeno hiyo kuisalimisha katika taasisi husika pamoja na kupiga marufuku ufugaji wa mifugo katika baadhi ya mitaa.

Katika zoezi hilo la kuzuia mifugo  kwa ngo’mbe atakapokamatwa atalipishwa shilingi laki 3 mbuzi na kondoo faini laki moja ambapo pia mmiliki atalazimika kulipa shilingi elfu tano kwa siku kwa ajili ya  utunzaji wa wanayama hao.