JUHUDI ZINAHITAJIKA ILI WANANCHI KUONDOKANA NA KADHIA

 

Licha ya  juhudi  zinazochukuliwa na vingozi  za kutatua  changamoto  ya maji katika  shehiya   lakini   bado  juhudi  zinahitajika   ili  wananchi  kuondokana  na kadhia  hiyo.

Wakizungumza baada  ya kukabidhiwa  matangi ya kuhifadhia maji   baadhi ya wakaazi wameeleza kuwa  wana matumaini  ya kupata  huduma hiyo  hiyo  ipasavyo  kwa sasa  huku  wakiwaomba viongozi hao  kutoa  ushirikiano ili  kuhakikisha huduma  hiyo  inapatikana   ipasvyo   bila  kusua sua .

Akikabidhi vifaa mbali mbali katika jimbo hilo  vikiwemo mashine za za kupima  presha na  sukari pamoja matangi   sita vyenye thamni ya shilingi  milioni nane  katika shehiya ziliomo  humo   mwakilishi wa jimbo la mtoni  mh: ibrahim  makungu amewasisiza wananchi   kutumia huduma hiyo bila ubaguzi kama ilani ya chama inavyoelekeza  ili kufikia  maendeleo  kwa wote .

Amesema atahakikisha maendeleo  ya msingi  yanawafikia wananchi wote  ikiwemo  elimu , afya na huduma ya maji  katika jimbo  hilo  yote matatizo  yanayowakabili   ili  waondokane na usumbufu