JUMLA YA MATUKIO 440 YA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA YAMEGUNDULIKA KATIKA TAFITI YA KIHABARI

Jumla ya matukio 440 ya udhalilishaji wa kijinsia yamegundulika katika tafiti ya kihabari iliyofanywa na chama cha waandishi wa habari wanawake tamwa zanzibar.
Utafiti huo umeonyesha matukio mbali mbali ya udhalilishaji yakiwemo ya ubakaji, ulawiti,na utoroshaji wa watoto.
Mshauri wa vyombo vya habari na mtafiti kutoka tamwa nd ali sultani akitoa maelezo juu ya utafiti huo katika kongamano la siku kumi na sita la kupinga udhalilishaji lililofanyika waeles kikwajuni amesema juu ya utafiti huo lakini elimu zaid inahitajika kwa jamii ili kuondosha kabisa vitendo hivyo.
hakimu wa mahakama ya watoto mwera hakimu naila abdul basit ametoa wito kwa jamii kuongeza ushirikiano na vyombo ya sheria ili kutokomeza vitendo vya udhalilishaji.
Washiriki wa kongamano hilo ambalo limetayarishwa na tamwa wana haya yakueleze
Madada mbali mbali zimewasilishwa katika kongamano hilo ambapo mwenyekiti wa kongamano hilo bi asha aboud amesema lengo la kongamano hilo ni kutoa fursa kwa jami kutoa maoni yao juu ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji kuondoshwa kabisa.