JUMLA YA SH 425,541,000/= ZIMEPATIKANA KUFUATILIA ZOEZI LA UKODISHWAJI WA MASHAMBA YA KARAFUU

Jumla ya shilingi milioni mia 425,541,000/= zimepatikana kufuatilia zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya karafuu 274 ya serikali linaloendelea katika Wilaya ya Wete.

Tathmini hiyo imebainika kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman wakati akikagua zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya karafuu ya serikali katika bonde la Mtong’ombe shehia ya Mtamwe Kusini wilaya ya Wete.

Akizungumza na wananchi hao wakati wa mnada wa ukodishwaji Mh. Omar amewataka watendaji walioteuliwa kusimamia zoezi hilo kuwa waadilifu na kuhakikisha hawafanyi upendeleo katika kazi hiyo.

Akitowa taarifa ya ukodishwaji wa mashamba hayo, Kaimu Afisa Mdhamini wizar ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Issa Nassor amesema tayari mashamba 274 yameshakodishwa kwa wananchi.

Msimamizi wa zoezi hilo Hamad Omar amesema changamoto kubwa inayowakumba ni kwa wanyeji wa mashamba kutoonesha mipaka halisi ya mashamba hayo.

Zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya mikarafuu linaendelea wilaya ya Wete na litafanyika katika wilaya ya Micheweni.