JUMLA YA SHILINGI BILIONI KUMI ZIMETENGWA KWA AJILI YA MALIPO YA ZIADA YA PENCHENI

Waziri wa fedha na mipango dk khalid mohamed salum amesema serikali imefanya mapitio ya kima cha chini cha pencheni kwa kima cha sasa kimepitwa na wakati kutokana na kupanda gharama za maisha.
Amesema jumla ya shilingi bilioni kumi zimetengwa kwa ajili ya malipo ya ziada ya pencheni kutokana na viwango vipya vilivyopangwa kutumika mwaka mpya wa fedha wa mwaka 2017 utakapoanza.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 207/2018 dk khalid amefahamisha kuwa mapitio hayo yamezingatia pia wastaafu waliokuwa na nyadhifa serikalini ambao kwa sasa wanapokea kiwango kidogo cha pencheni kutokana na mishahara midogo waliomaliza utumishi wao.
Amesema kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 wizara ya fedha imependekeza kuwa na kiwango cha usajili wa namba hizo kwa gari zilizopo kwa usajili mpya kuwa shilingi milioni 15 kwa mwaka badala ya kiwango cha sasa cha shilingi milioni 3 kwa miaka 3.
Wajumbe wa baraza la wawakilishi pamoja na makamu wa pili wa rais mh. Balozi seif ali iddi walitoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo na kufahamisha kuwa imekidhi mahitaji mengi
Wizara hiyo hiyo imeomba kuidhinishiwa mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo serikali imekusudia kukusanya shilingi trilioni moja, bilioni thamanini na saba na milioni mia nne .