JUMUIYA YA MAENDELEO YA VIJANA IMEANZA MRADI VIJANA KUJIUNGA NA VYUO VYA AMALI

 

Jumuiya ya maendeleo ya vijana ya Mikunguni imeanza mradi wa kuhamasaisha vijana kujiunga na vyuo vya amali ili kuweza kujiajiri na kuondokana na utegemezi.

mradi huo awamu ya pili wa elimu mbadala na mafunzo ya amali unasimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali unalenga kufika vijana wa wilaya zote za zanzibar amenza kutoa elimu kwa vijana wa wilaya ya magharibi a.

asma ali kutoka jumuiya ya Maydo ameeleza namana ya mradi huo utakavyotelezwa ikiwemo kuhamasisha kundi hilo kupenda kusoma.

Mwakilishi wa jimbo la kwahani Mh Ali Salum amezungumza na vijana waliopatiwa mafunzo hayo kutoka wilaya ya Magharibi a  na kuwataka kubuni mbinu  zaidi za kijiendeleza kimaisha.

baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo hayo wameelezea kufarijika baada ya kupatiwa mafunzo hayo na kuomba kuendelea kutolea kila mara.