JUMUIYA YA ZEDO YATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA NCHI

Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mh Hemed Suleiman Abdallad ameitaka Jumuiya ya maendeleo ya kielimu Zanzibar  zedo kufuata sheria na kanuni za nchi katika utoaji wa mikopo kwa wajasiri amali ili kuweza kuepukana na migogoro kati yao na wajasiri amali hao.

Mh Hemed ameitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanachama wa zedo ambao ni wajasiri amali  juu ya uchukuaji  mkopo wa chap chap huko katika ukumbi wa Samail Gombani chake chake pemba

Mh Hemed amesema ni lazima kwa jumuiya au taasisi kufuata sheria na kanuni ili kuweza kuondoa ubabaishaji  kwa wanachama wake sambamba na kuwataka wanachama hao kuitumia mikopo watakayoipata katika kupambana na umasikini na kijienua kiuchumi pamoja na kuwataka kurejesha mikopo hiyo kw awakati ili kuweza kutoa fursa kwa wanachama wengine kupata mikopo hiyo

Nae  mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya elimu Zanzibar  zedo ambae pia ni mkurugenzi wa mfuko wa mikopo nd ussi said suleiman amesema zedo imeanzisha mkopo wa chap chap kwa ajili ya wajasiri amali wadogo wadogo ili kuweza kuendeleza shughuli zao

Nao wanachama wa zedo ambao ni wajasiri amali wameziomba taasisi za kifedha zikiwemo bank kuweza kupunguza masharti ya uchukuaji wa mikopo kwa wajasiri amali wadogo wadogo .

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App