JUMUIYA ZISIZO ZA KISERIKALI KUONGEZA USHIRIKIANO DHIDI YA MAPAMBANO YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

Jumuiya zisizo za kiserikali zimetakiwa kuongeza ushirikiano dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu ili kuhakikisha unatokomea kabisa na zanzibar.
Wito huo umetolewa na mratib wa kifua kikuu , ukoma na ukimwi zanziba dr. Khamis abubakar suleiman wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka jumuiya zisizo za kiserikali ambazo zinashirikiana na kitengo shirikishi katika mapambano juu ya ugonjwa wa tb kwa lengo la kutathmini mafanikio na changamoto katika kipindi cha robo mwaka huko katika ukumbi wa samail gombani kisiwani pemba.
Mratib huyo amesema ugonjwa wa kifua kikuu zanzibar bado upo na unaendelea kuathiri watu ndio maana wakashirikiana na jumuiya nyengine zisizo za kiserikali kwa kuongeza nguvu katika mapambano hayo ili kuhakikisha ugonjwa huo unaondoka.
Nae mratib kitengo shirikishi upande wa kisiwani pemba dr. Hamad omar hamad amesema lengo la kuzishirikisha ngo’s ni kuhakikisha kwamba ugonjwa huo unagundulika mapema na watu waweze kupatiwa tiba mapema ili kuzuiya ongezego la gonjwa hilo.
Kwa upande wake hasina ali said ambae ni mshiriki wa mutano huo amesema.
Jumuiya ambazo zinashirikiana na kitengo shirikishi tb, ukoma na ukimwi kwa upande wa kisiwani pemba ni pamoja na zanzibar youth forum,mkupe,watoa huduma za majumbani hbc na pemba press club.