JUNCKER ASIFU MAKUBALIANO YA KUUNDA SERIKALI UJERUMANI

 

Rais wa halmashauri kuu ya umoja wa ulaya jean-claude juncker ameyakaribisha makubaliano ya kuunda serikali ya mseto nchini ujerumani kati ya vyama vya kihafidhina vya kansela angela merkel vya christian democratic union cdu, christian social unioni csu na kile cha kisoshalist cha social democratic spd.

Juncker amesema anakaribisha hatua ya serikali mpya ya ujerumani kuhusiana na dhamira iliyonayo katika masuala ya sera za umoja wa ulaya.

moja ya maeneo ambayo ameyataka ni dhamira ya vyama vya cdu/csu na spd kuongeza mchango wake katika bajeti ya umoja wa ulaya.

kansela merkel alilazimika kufanya maridhiano makubwa katika  majadiliano kuhusiana na mgawanyo wa nyadhifa za baraza la mawaziri ili kuweza kupatikana muafaka katika mazungumzo hayo ya kuunda serikali yaliyochukua muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kukubali kutoa wadhifa muhimu wa waziri wa mambo ya kigeni kwa chama cha spd, ambapo kiongozi wa chama hicho martin schulz anatajwa kuwa kiongozi wa wizara hiyo.