KADINALI PELL ASHTAKIWA KWA MAKOSA YA UNYANYASAJI KINGONO

Kadinali Pell ashtakiwa kwa makosa ya unyanyasaji kingono

polisi nchini Australia imesema imemfungulia mashtaka mkuu wa idara ya Fedha ya Vatican Kadinali George Pell kuhusiana na makosa kadhaa ya madai ya udhalilishaji.

wachunguzi kutoka jimbo la Victoria wamesema kulikuwa na malalamiko kadhaa kuhusiana na makosa ya zamani.

Pell, ambaye ni kiongozi wa ngazi ya juu wa kanisa katoliki nchini humo, amekanusha vikali madai hayo.

Kadinali Pell amekuwa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa vatican, kushitakiwa katika kashfa ya unyanyasaji kingono inayolikumba kanisa katoliki.